Monday, 3 June 2013

MWILI WA NGWEA KUWASILI KESHO SAA NANE MCHANA

Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Albert Mangweha tunapenda kuwaatarifu rasmi kuwa mwili wa marehemu Ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha utawasili kesho tarehe 04/06/2013 saa nane mchana na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Terminal One).
Tunaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kumpokea ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha.
Taarifa hii kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mapokezi na Mazishi. Asanteni na Mungu awabariki

No comments:

Post a Comment