Sunday, 2 June 2013

JE UNAFAHAMU KUHUSU MAFANIKIO YA DIAMOND PLATINUM?

Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinum kipenzi cha wengi, ni msanii anaeng'ara sana nchini Tanzania tangu alipoanza na single yake ya Mbagala mpaka hii leo bado anafanya vizuri tena zaidi ya jana, kiukweli jamaa amejipanga katika kila sector, anafanya Good Music na anabamba kila rika na kuwaburudisha vilivyo.
Diamond ni msanii anaepiga show nyingi sana na kwa malipo makubwa tofauti na mengine ambapo ili kuweza kumpata jamaa basi lazima ujipange na Milioni kadhaa kama 5 hivi kwa show moja na kwa sababu raia wanamkubali basi sio kesi wala pesa nyingi kwao, wadau wanaingia na kufanya nae mkataba, na inasemekana kuwa ana piga show kila week mara tatu mpaka nne sehemu tofauti tofauti. Na hivi juzi tu alitoka Kusini mwa Afrika kwa Madiba ndani ya mjengo wa Big Brother Africa kutumbuiza na kwa taarifa zisizo rasmi inasemekana jamaa alinyakua kitita cha Tanzania Milioni 30 kwa ajili ya show hiyo.
Pia ni msanii ambae ameweza kukutana na wasanii wengine wa Kimataifa






Huku akiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ni msanii wa kwanza kupiga show ya kipekee yenye kiingilio kikubwa, ilifanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambayo ili enda kwa jina la "DIAMOND FOREVER".
Furaha ndio kitu kikubwa maishani
Ila kuna yale maneno ya jamaa wakisema kuwa Diamond ni mwanachama wa Freemasons, ukweli anaujua yeye so kama amesema sio basi sio raia acheni maneno ila mnatakiwa mumpe support ili azidi kufanya fresh
Msosi kitu muhimu aaaah! freeeeeeeeeeeeesh sana.

Kikubwa katika mafanikio yake ni juhudi na kujiamini pia kutokukata tamaa, Kwa wasanii wote inawapasa kuwa na ujasiri na roho ya kupenda maendeleo na sio kulewa sifa kidogo ukajiona bonge la star ama kwenda kuuza habari kwenye gazeti ili uonekane Topic kila cku hiyo ni mbaya maana inashusha hadhi yako. Chakarika ule kwa jasho lako na sio kusubiri vimeo vikutoe.

No comments:

Post a Comment